Design March 10, 2026

Jinsi rangi za ndani zinavyoweza kubadili muonekano wa sebule yako.

Site Visit

Rangi siyo tu urembo; ni hisia. Mwaka 2026, tunaona mabadiliko makubwa katika uchaguzi wa rangi za ndani (Interior Colors).

Watu wengi wanaogopa kutumia rangi nzito kama "Navy Blue" au "Charcoal Grey", lakini siri ya kisasa ni mchanganyiko (Contrast). Ukichanganya ukuta mmoja wa rangi nzito na kuta nyingine za rangi ya "Cream" au "Off-white", unapata sebule inayonekana ya kifahari (Luxury look).

"Siri ya nyumba nzuri haipo kwenye fanicha za bei mbaya, bali kwenye mpangilio wa rangi na mwanga (Lighting)."

Umuhimu wa Mwanga wa Asili

Blessedhand tunasisitiza matumizi ya madirisha makubwa. Mwanga wa jua ukikutana na rangi sahihi, hufanya chumba kionekane kikubwa kuliko kilivyo. Pia, kuweka vioo (Mirrors) kwenye kuta kunasaidia kuakisi mwanga na kuleta hali ya upana.

Share this insight